<-
8<
>10 LANG:
CD/ANUNCIATE

Luka 9

Yesu Awatuma Wanafunzi Kumi Na wawili
 1Yesu akawaita pamoja wanafunzi wake kumi na wawili na kuwapa mamlaka na uwezo wa kufukuza pepo wote na kuponya magonjwa yote. 2Kisha akawatuma waende wakautangaze Ufalme wa Mungu na kuponya wagonjwa.

 3Akawaagiza akisema, ``Msichukue cho chote safarini, wala fimbo, wala mkoba, wala chakula, wala fedha; na msichukue nguo za kubadili. 4Mkikaribishwa katika nyumba yo yote muwe wageni wa nyumba hiyo hadi mtakapoondoka katika kijiji hicho. 5Po pote ambapo hamtakaribishwa, mnapoondoka kung'uteni mavumbi miguuni mwenu kama ishara ya hukumu ya Mungu juu yao.''

 6Wale wanafunzi wakaondoka wakaenda kutoka kijiji hadi kijiji wakihubiri Habari Njema na kuponya wagonjwa. 7Habari zil imfikia Herode mtawala wa Galilaya kuhusu miujiza iliyokuwa iki fanyika, naye akafadhaika kwa kuwa baadhi ya watu walikuwa wakisema, ``Yohana Mbatizaji amefufuka!'' 8Wengine wakasema, ``Ni Eliya ametutokea'' na wengine kwamba, ``Mmoja wa manabii wa kale amefufuka.'' 9 Herode akasema, ``Yohana nilimkata kichwa, ni nani huyu anayefanya maajabu haya ninayoambiwa?'' Akajaribu sana amwone Yesu.

Yesu Awalisha Watu Elfu Tano
 10Wanafunzi waliporudi walimweleza Yesu yote waliyofanya. Akawachukua wakaenda peke yao mpaka mji mmoja uitwao Bethsaida. 11Lakini watu wengi wakafahamu alipokwenda, wakamfuata. Akawa karibisha, akawafundisha tena kuhusu Ufalme wa mbinguni na akapo nya wangonjwa. 12Ilipokaribia jioni, wale wanafunzi kumi na wawili wakamwambia Yesu, ``Waruhusu watu hawa waondoke ili waweze kujitafutia chakula na mahali pa kulala katika vijiji na mashamba ya jirani kwa maana hapa tuko nyikani.'' 13Akawajibu, ``Wapeni chakula.'' Wakasema, ``Tunayo mikate mitano tu na samaki wawili. Unataka tukanunue chakula cha kuwatosha watu wote hawa?'' 14 Kwa kuwa walikuwapo wanaume wapatao elfu tano! Lakini Yesu akawaambia wanafunzi wake, ``Waketisheni katika makundi ya watu hamsini-hamsini.'' 15Wakawaketisha wote. 16Yesu akaichukua mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama mbinguni, akavi bariki na kuvimega. Kisha akawapa wanafunzi wake wawagawie wale watu. 17 Kila mtu akala na kutosheka na vilipokusanywa vipande vilivyobaki, vilijaa vikapu kumi na viwili.
Petro Amkiri Bwana Yesu Kuwa Ndiye Kristo
 18Siku moja Yesu alipokuwa akisali faraghani akiwa na wana funzi wake aliwauliza, ``Watu husema mimi ni nani?'' 19 Wakam wambia, ``Watu husema wewe ni Yohana Mbatizaji, wengine husema ni Eliya na wengine husema wewe ni nabii wa kale aliyefufuka kutoka kwa wafu.''

 20Kisha akawauliza, ``Ninyi je, mnasema mimi ni nani?'' Petro akajibu, ``Wewe ndiye Kristo wa Mungu.'' 21 Yesu akawaka taza wasimwambie mtu jambo hilo 22akisema, ``Imenipasa mimi Mwana wa Adamu kupata mateso mengi na kukataliwa na wazee, maku hani wakuu na walimu wa sheria. Nitauawa na siku ya tatu nitafuf uliwa.'' 23Kisha akawaambia wote, ``Ye yote anayetaka kunifuata ni lazima ajikane nafsi yake, achukue msalaba wake kila siku, anifuate. 24Kwa maana ye yote atakayeshughulikia zaidi usalama wa nafsi yake ataipoteza. Lakini ye yote atakayeipoteza nafsi yake kwa ajili yangu ataisalimisha. 25Je, kuna faida gani kwa mtu kuupata ulimwengu mzima ambapo kwa kufanya hivyo ataipoteza nafsi yake? 26Mtu ye yote atakayenionea aibu mimi na maneno yangu, na mimi Mwana wa Adamu nitamwonea aibu mtu huyo nitakapo kuja katika utukufu wangu na wa Baba na wa malaika watakatifu. 27Ninawaambia kweli, baadhi ya watu waliosimama hapa hawatakufa mpaka watakapouona Ufalme wa Mungu.''

Bwana Yesu Abadilika Sura
 28Yapata siku nane baada ya kusema hayo, Yesu alikwenda kusali mlimani pamoja na Petro, Yakobo na Yohana. 29 Alipokuwa akiomba, sura yake ili badilika, mavazi yake yakawa meupe, yakimetameta na kung'aa. 30Ghafla wakawepo watu wawili wakaanza kuzungumza naye. Walikuwa ni Musa na Eliya! 31Nao walionekana katika utukufu wakizungumza na Yesu kuhusu kifo chake ambacho kingetokea Yerusalemu.

 32Petro na wenzake ambao walikuwa wamelala usingizi mzito waliamka wakaona utukufu wa Yesu na wale watu wawili waliokuwa wamesimama pamoja naye. 33Musa na Eliya walipoanza kuondoka, Petro akamwambia Yesu, ``Bwana ni vizuri mno kwamba tuko hapa! Tutajenga vibanda vitatu - kimoja chako, kingine cha Musa na kin gine cha Eliya.'' Lakini Petro hakujua anasema nini. 34Petro alipokuwa bado anazungumza, pakatokea wingu kubwa na kivuli chake kikawafunika, na wale wanafunzi wakashikwa na hofu lile wingu lilipowafikia. 35Sauti ikatoka kwenye wingu ikisema, ``Huyu ni Mwanangu niliyemchagua, msikilizeni yeye.'' 36Baada ya sauti hiyo kusema, alionekana Yesu peke yake. Wale wanafunzi wakakaa kimya na kwa wakati huo hawakumwambia mtu ye yote yale waliyoy aona.

 37Kesho yake aliposhuka kutoka mlimani alikutana na umati mkubwa wa watu. 38Ghafla, mtu mmoja kati yao akapiga kelele akasema, ``Mwalimu, tafadhali nakuomba umwangalie mtoto wangu, ni mwanangu wa pekee. 39 Mara kwa mara pepo humshika na kumfanya apige kelele kisha humwangusha na kumtia kifafa akatokwa na povu mdomoni. Anamtesa sana na hamwachii ila kwa shida. 40Nimewaomba wanafunzi wako wamwondoe huyo pepo lakini wameshindwa.'' 41Yesu akajibu, ``Enyi watu mliopotoka, msio na imani, nitakaa nanyi na kuwavumilia mpaka lini? Mlete mwanao hapa.''

 42Yule mtoto alipokuwa akija, yule pepo akamwangusha, akam tia kifafa. Lakini Yesu akamwamuru yule pepo amtoke. Akamponya yule mtoto akamkabidhi kwa baba yake. 43Watu wote walishangaa walipoona huo uweza mkuu wa Mungu. Wakati watu walipokuwa wanas taajabia hayo yote aliyokuwa akiyafanya Yesu, yeye aliwaambia wanafunzi wake: 44`` Sikilizeni kwa makini haya nitakayowaambia sasa: mimi Mwana wa Adamu nitasalitiwa na kuwekwa mikononi mwa wanadamu.'' 45Lakini wanafunzi wake hawakuyaelewa maneno hayo. Maana ya maneno hayo ilikuwa imefichwa ili wasiweze kuelewa, nao waliogopa kumwuliza.

Yesu Afundisha Kuhusu Ukubwa
 46Wanafunzi wakaanza kubishana wao kwa wao kuhusu nani kati yao alikuwa mkuu zaidi. 47Lakini Yesu aliyatambua mawazo yao, akamsimamisha mtoto mdogo karibu naye 48kisha akawaambia, ``Ye yote atakayemkaribisha mtoto huyu mdogo kwa jina langu atakuwa amenikaribisha; na ye yote atakayenikaribisha mimi atakuwa amem karibisha yeye aliyenituma; kwa maana yeye aliye mdogo kati yenu, ndiye aliye mkubwa kuliko wote.'' 49 Yohana akasema, ``Bwana, tumemwona mtu akifukuza pepo kwa jina lako tukamzuia kwa maana yeye si mmoja wetu.'' 50Yesu akasema, ``Msimzuie kwa sababu ye yote ambaye hapingani nanyi, yuko upande wenu.''
Yesu Akataliwa Samaria
 51Siku zake za kurudi mbinguni zilipokaribia, Yesu aliamua kwamba lazima aende Yerusalemu na akaanza safari kuelekea huko. 52Akatuma watu wamtangulie, nao wakaenda katika kijiji kimoja cha Samaria kumwandalia kila kitu. 53Lakini watu wa kijiji hicho walikataa kumpokea kwa sababu ilikuwa dhahiri kwamba ali kuwa anakwenda Yerusalemu. 54Basi wanafunzi wake Yakobo na Yohana walipoona hayo, wakasema: ``Bwana, unataka tuamuru moto kutoka mbinguni uwaangamize?'' 55Yesu akageuka, akawakemea. 56Wakaenda kijiji kingine.
Gharama Ya Kumfuata Yesu
 57Walipokuwa wakienda, mtu mmoja akamwambia Yesu, ``Nitakufu ata po pote utakapokwenda.'' 58Yesu akamwambia, ``Mbweha wanaishi kwenye mapango yao na ndege kwenye viota vyao lakini mimi Mwana wa Adamu sina mahali pa kulala na kupumzika.''

 59Yesu alimwambia mtu mwingine, ``Nifuate.'' Mtu huyo akamjibu, ``Bwana, niache kwanza nikamzike baba yangu.'' 60Yesu akamwam bia, ``Waache wafu wawazike wafu wao. Bali wewe nenda ukautan gaze Ufalme wa Mungu.'' 61Mtu mwingine akamwambia, ``Bwana nitakufuata lakini naomba kwanza nikaage jamaa yangu.'' 62Yesu akamwambia, ``Mtu ye yote ashikaye jembe kuanza kulima kisha akawa anageuka kutazama nyuma, hafai kwa Ufalme wa Mungu.'' Yesu Awatuma Wafuasi Sabini na Wawili




VOLVER

(c) Swahili New Testament, de sus respectivos autores. ¿Deseas Colaborar o Retribuir?. ¿Deseas Comprar el disco y la audiobiblia en mp3? *Ninguna version de descarga tiene publicidad. Si deseas anunciarte gratis haz click aqui. Empyreon Technology